Kaimu Posta Masta Mkuu wa TPC, Fortunatus Kapinga |
Kaimu Posta Masta Mkuu wa shirika hilo, Fortunatus Kapinga alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana katika maadhimisho ya Siku ya Posta barani Afrika.
Kapinga alisema mbali na maboresho hayo huduma hizo zitapanuliwa katika mikoa mingi zaidi nchini ikiwemo Kilimanjaro, Arusha, Tanga, Morogoro, Iringa, Mbeya, Lindi na Mtwara ili kuongeza ufanisi katika maeneo hayo.
“Huduma hii ambayo inatoa hakikisho la wananchi kufikishiwa bidhaa zao ndani ya saa 24, kwa sasa inahudumia mikoa iliyounganishwa na barabara kuu za Dar es Salaam kwenda kaskazini, kati na Nyanda za Juu Kusini,” alisema Kapinga.