February 20 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam klabu kongwe na zenye upinzani Tanzania Simba na Yanga zitashuka dimbani kupambana katika mchezo wao wa marudiano wa mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara, hivyo presha na idadi kubwa ya watu inategemewa kujaa uwanja wa Taifa.
Kufuatia mchezo huo kuwa na utamaduni wa kujaza idadi kubwa ya mashabiki, shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza utaratibu wa kufunga barabara ya kuanzia DUCE kuelekea uwanja wa Taifa na hivyo inaomba mashabiki na watu watumie upande wa barabara ya Mandela kuingia Taifa na maeneo jirani, kwani magari hayataweza kukatisha. Tiketi za mchezo huo zimeshaanza kuuzwa katika vituo vilivyotangazwa.